Dayna Nyange:Juhudi bila ya Wadau ngumu kutoboa nje

Juhudi bila ya Wadau ngumu kutoboa nje – Dayna Nyange. 

Mwanamuziki Dayna Nyange ametoa mtazamo wake wa namna gani wasanii wa nyumbani watawezakuvuka mipaka ya nje ya nchi

Alipokuwa anafanyiwa mahojiano na mwandishi wa habari hii Dayna alifunguka kwamba ili wasanii waweze kutoboa ni lazima wawe na Wadau wa nje (connection) kwani wengi wanafanya kazi nzuri lakini kutokuwa na wadau ndio kikwazo.

“Msanii kama Vanessa Mdee leo hii anaanza kuvuka boda ni kwa sababu ya connection ya watu wa nje alionao, kama aliweza kufanya kazi na watu wa MTV sasa kwa nini asifike mbali ukizingatia anafanya kitu kizuri”, alifafanua Dayna.

Dayna alieleza pia kuhusu ujio wa video ya wimbo wake wa Nitulize aliomshirikisha Nay wa Mitego kwamba wataanza kuirekodi siku chache zijazo kwani kuna vitu muhimu wanasubiri kutoka nje ya nchi.

Video hiyo inatarajiwa kurekodiwa hapahapa nyumbani Tanzania, huku akisita kuweka wazi ni kampuni gani ambayo itatengeneza video hiyo na kusema watu wasubiri Surprise.

Dayna mwanamuziki huyu mwenye asili ya mkoani Morogoro mwisho alitoa taarifa kwa mashabiki wake wa Tanga wakae sawa kwani anatarajia kuanza show zake mkoani humo kuanzia sikukuu ya Eid.


0 comments: